KIPA MPYA SIMBA RIPOTI YA DAKTARI STARS KUTOA MAAMUZI

UONGOZI wa Klabu ya Simba unaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya makipa wake wawili, Yakoub Seleman na Moussa Pinpin Camara, ukisubiri  ripoti ya daktari wa Taifa Stars itakayobainisha hali halisi ya Yakoub ambaye amekuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha.

Ripoti hiyo ya kitabibu inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika maamuzi ya kiufundi ya klabu, hasa ikizingatiwa kuwa Yakoub ni miongoni mwa makipa tegemeo ndani ya kikosi cha Simba katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Sambamba na hilo, uongozi wa Simba pia unaangazia maendeleo ya kiafya ya  Camara,  naye amekuwa akikabiliwa na changamoto za majeraha, hali inayozua sintofahamu juu ya upatikanaji wake katika michezo ijayo.

Baada ya kupokea ripoti zote mbili, uongozi unatarajiwa kukaa mezani na kocha mkuu wa timu hiyo, Steve Barker, kwa lengo la kufanya tathmini ya kina kuhusu hali ya makipa hao na mwelekeo wa timu katika kipindi kijacho.

Endapo ripoti hizo zitabainisha kuwa Yakoub  na  Camara watakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu kuanzia sasa, Simba italazimika kufanya maamuzi mazito ili kulinda maslahi ya timu na ushindani wake.

Moja ya chaguo linaloangaliwa ni kuingia sokoni kusaka kipa mpya atakayeziba pengo hilo kwa muda au hata kwa muda mrefu kulingana na hali itakavyoonekana, jambo ambalo litahitaji maamuzi ya haraka kutoka kwa uongozi.

Hata hivyo, chaguo jingine ni kuendelea kuwaamini makipa waliopo, hususan Hussein Abel, ambaye anaweza kupewa jukumu kubwa la kuilinda lango la Simba katika kipindi hiki kigumu, huku klabu ikisubiri urejeo wa makipa wake wakuu.

The post KIPA MPYA SIMBA RIPOTI YA DAKTARI STARS KUTOA MAAMUZI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/EznbLe1
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post