Imma, kijana fundi magari kutoka Temeke, alikuwa na kipaji kikubwa cha kutengeneza injini, kusuka umeme wa magari na kugundua hitilafu ambazo mafundi wengi walishindwa kuzitambua. Alianza kujifunza fani hiyo tangu akiwa mdogo kwenye gereji ya jirani na alipoingia utu uzima, ndoto yake ilikuwa kuwa fundi anayeheshimiwa na kupata kipato kizuri kutokana na ujuzi wake. Hata hivyo, maisha hayakumwendea kama alivyotarajia. Alikuwa akihangaika kupata kazi yenye malipo mazuri, licha ya kuwa na ufundi wa hali ya juu. Mara nyingi alipata vibarua vidogo visivyo na uhakika, vingine vikiwa na malipo kidogo sana ambayo hayakuweza kumudu mahitaji yake ya kila siku.
Miaka ilivyopita, Imma alianza kukata tamaa. Aliwahi kuomba kazi kwenye gereji kubwa na kampuni za usafirishaji, lakini mara nyingi aliambiwa “tutakupigia baadaye” bila kupigiwa. Wakati mwingine aliitwa kufanya kazi ngumu ya siku nzima, lakini mwisho wa siku akapewa malipo yasiyolingana na kazi aliyoifanya. Marafiki zake wengi walimshauri abadilishe fani, lakini moyo wake ulizidi kumwambia kuwa ufundi ni kipaji chake cha kweli. Hata hivyo, kadiri maisha yalivyozidi kuwa magumu, alihisi kama vile kuna kitu kinamzuia kupiga hatua kubwa zaidi. Soma zaidi hapa

Post a Comment