AHMEDY ALLY ATOBOA KOCHA WA SIMBA KUJA JANUARY

UONGOZI wa Klabu ya Simba umethibitisha kuwa mchakato wa kumpata kocha mpya unaendelea kwa kasi, na kabla ya Januari 2026 jina la atakayekabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo litajulikana rasmi.

Hii inalenga kumpa muda wa kutosha kujiandaa na kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu ujao na michuano ya kimataifa.

Simba ilijikuta ikihitaji kocha mpya baada ya kumtimua Dimitar Pantev, aliyekuwa amepewa majukumu ya uendeshaji wa timu kwa siku 61 pekee.

Uongozi unasema uamuzi huo ulilenga kuleta mabadiliko chanya na kuhakikisha timu inarejea kwenye ushindani mkubwa ndani na nje ya nchi.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema tayari wamepokea wasifu (CV) nyingi za makocha kutoka mataifa mbalimbali, uchambuzi wa kina unaendelea ili kumpata kocha mwenye hadhi na uwezo wanaoutaka.

Kwa mujibu wake, klabu inalenga kumtangaza kocha huyo kabla ya mwezi Januari ili aweze kuanza kupanga mipango na mbinu za msimu mapema.

“Baada ya mchezo wetu wa leo dhidi ya Azam FC, timu itaenda mapumziko mafupi. Tunatarajia kocha mpya atapata muda wa wiki tatu hadi nne kukaa na timu kabla ya mechi yetu ya kimataifa,” amesema Ahmed,

Ameongeza kuwa kocha mpya atapewa programu ya wiki nne za maandalizi (pre-season) kabla ya kuanza majukumu yake rasmi.

Simba imeweka malengo ya kuhakikisha kila kitu kinakuwa tayari ifikapo Januari 23, 2026, siku ambayo itashuka dimbani kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Esperance Sportive de Tunis katika michuano ya kimataifa.

Ingawa jina la kocha halijatangazwa wazi, taarifa za ndani zimeeleza kuwa Simba ipo katika mazungumzo ya karibu na kocha mzaliwa wa Barcelona, Antonio ‘Toni’ Cosano Cantos, mwenye umri wa miaka 48, ambaye aliwahi kuinoa Petro Atletico ya Angola.

Endapo mazungumzo yatakamilika vyema, Cosano anaweza kutangazwa kuwa kocha mpya wa Msimbazi kabla ya kuanza kwa mechi za Ligi Kuu na zile za CAF.

The post AHMEDY ALLY ATOBOA KOCHA WA SIMBA KUJA JANUARY appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/izmNqnr
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post