Yanga Yatangaza Ratiba Wiki ya Mwananchi

 


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametangaza ratiba ya matukio ambayo yatafanywa na klabu hiyo kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi Ijumaa hii Septemba 12

Akizungumza na wanahabari Serena Hotel mapema leo, Kamwe aliwataka wanachama na mashabiki kushiriki katika matukio hayo kwenye maeneo yao

“Leo tunatoa ratiba ya wiki ya mwananchi. Jambo lolote ambalo litafanywa Dar na litapaswa kufanywa na mashabiki au wanachama wetu kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Kinachofanyika Mbagala au Tegeta, linapaswa kufanywa na wanachama wetu waliopo Tokyo, Lubumbashi, Pretoria, New York na Mombasa”

 “Kesho Jumanne tutakuwa na zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya matukio yetu ya wiki ya wananchi. Kituo chetu kikuu ni Makao makuu ya Klabu yetu Jangwani. Lakini tunawaomba wanachama wetu kuchangia damu katika hospital iliyopo karibu nawe. Kuna thamani kubwa sana ya chupa yako ya damu katika kuokoa maisha”

“Watu watakaochangia damu watapewa zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini wetu. Baada ya kuchangisha damu tutapata supu kama kawaida yetu. Tunapata supu huku tukijadiliana namna tutakwenda kilele cha wiki ya mwananchi tukiwa na vibe”

“Siku ya Jumatano tutakuwa na DUA maalumu. Lakini tunatamani kila mkoa mwanachama wa Yanga kwa imani tofauti tofauti wanapaswa kufanya dua kwenye maeneo yao. Dua hiyo itapaswa kufanywa mchana, ili tumuombe Mungu baraka zake ili atujalie mafanikio tele. Kitaifa dua hii itafanyika makao makuu ya klabu. Wote mnakaribishwa”

“Alhamis tutakuwa na charity katika hospital ya Muhimbili. Wanayanga wanapaswa kufika hospitali hiyo tukiwa na mahitaji mbalimbali. Kwa wale ambao hawataweza kufika muhimbili basi wanapaswa kwenda kwenye vituo mbalimbali na kuwafikia wahitaji,” alisema Kamwe

Wadhamini wakuu wa Yanga kampuni ya SportPesa na GSM, Haier, watashiriki bega kwa bega na Wananchi katika matukio hayo ya kurejesha kwa Jamii

Usikose kutazama Matamasha hayo na  Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post