Mshambuliaji hatari wa Simba SC, Steven Mukwala raia wa Uganda, huenda akaendelea kusalia Msimbazi licha ya klabu ya Al Ittihad ya Libya kuweka ofa nono mezani kwa ajili ya kumnasa, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa, Al Ittihad iliwasilisha dau la takribani dola milioni 1 (sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2.5 za Kitanzania) ili kumsajili straika huyo ambaye msimu uliopita aliifungia Simba mabao 13 kwenye ligi
Hata hivyo, ingawa uongozi wa Simba ulikuwa tayari kumuuza Mukwala, kocha mkuu Fadlu Davids aliweka msimamo kuwa hawana budi kumpata mbadala wake kwanza kabla ya kukubali dili hilo.
Lakini hadi kufikia majira ya saa 5:59 usiku jana, muda mchache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, hakukuwa na taarifa zozote za ujio wa nyota mpya, licha ya Simba kuhusishwa na kiungo mshambuliaji wa Vipers FC, Allan Okello.
Kumbuka kuwa tayari Simba imeshauza mshambuliaji Lionel Ateba, hali inayofanya kikosi hicho kubaki na washambuliaji watatu tegemeo Jonathan Sowah, Selemani Mwalimu na Steven Mukwala mwenyewe.
Endapo Mukwala ataondoka, Simba watalazimika kuwategemea zaidi Sowah na Mwalimu katika safu ya ushambuliaji, wakati timu ikikabiliwa na mashindano mengi msimu ujao
Japo dirisha la usajili Libya bado halijafungwa lakini kwa sasa Simba haitakuwa na nafasi ya kusajili mbadala wake kwa kuwa dirisha la ndani limefungwa
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au Bonyeza HApa Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

Post a Comment