Klabu ya Simba italazimika kucheza bila ya mashabiki mechi ya mkondo wa pili hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Gaborone United
Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Francistown huko Botswana, Jumapili Septemba 28 Simba itakuwa mwenyeji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 10 jioni
Simba ilikata rufaa kwa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) juu ya adhabu ya kuzuiwa kuingiza mashabiki katika mchezo huo, hata hivyo rufaa hiyo imekataliwa
Wekundu hao wa Msimbazi waliadhibiwa kufuatia matukio yaliyojitokeza msimu uliopita katika mchezo wa robo fainali CAFCC dhidi ya Al Masry ambapo mashabiki walivamia uwanja baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 na kutinga nusu fainali
Simba inahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare katika mchezo huo siku ya Jumapili ili kufuzu raundi ya kwanza
Mchongo huu hapa usikose kutazama mechi hizi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au Bonyeza HApa Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

Post a Comment