Jana Yanga ilianza vyema msimu wa ligi kuu ya NBC 2025/26 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Lassine Kouma, Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya aliyeingia mchezoni katika kipindi cha pili
Katika mchezo huo, mkufunzi wa Yanga Romain Folz alifanya mabadiliko ya kikosi chake akiwaanzisha baadhi ya nyota wapya kama Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr', Moussa Balla Conte, Kouma, Edmund John, Celestin Ecua na Andy Boyeli
Folz aliweka wazi umuhimu wa kufanya 'rotation' katika kikosi chake kutokana na ukaribu wa mechi kwani katika kipindi cha siku 8 Yanga imecheza mechi tatu na inakabiliwa na mechi ya ligi ya mabingwa siku ya Jumamosi
Hata hivyo unaweza kusema ni kama presha ya mchezo iliwazidi baadhi ya nyota wapya wakionekana kucheza chini ya kiwango
Folz alilazimika kufanya mabadiliko ya mapema katika kipindi cha pili akiwaingiza Mahamed Doumbia na Aziz Andabwile ambao kwa kiasi kikubwa waliimarisha safu ya kiungo, kabla ya Pacome Zouzoua, Prince Dube na Mudathir Yahya kuongeza makali zaidi baada ya kuingia
Ni wazi baadhi ya nyota wapya bado wanahitaji muda zaidi ili kuweza kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza
Mpaka sasa Edmund John, Zimbwe Jr, Kouma na Doumbia ndio wanaonekana kufanya vyema zaidi miongoni mwa nyota wapya
Usikose kuitazama mechi ya SIMBA VS FOUNTAIN GATE LIVE kupitia Simu yako pia ukiwa na app hii utaweza kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au Bonyeza HApa Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

Post a Comment