Mzee Juma alikuwa mwanamume mnyenyekevu mwenye umri wa miaka 62. Maisha yake yote yamekuwa ya kujituma kwa jasho, kwani hakuwa na elimu kubwa ya kumwezesha kufanya kazi za ofisini. Hivyo, kazi ya ulinzi ndiyo ikawa tegemeo lake kuu katika kulea familia yake. Alichukuliwa na kampuni moja ya usalama mjini Mwanza, na kwa zaidi ya miaka kumi alihesabika kama mlinzi mwaminifu na mchapakazi.
Siku moja, usiku wa manane akiwa kazini, mauti yalimpita kwa macho. Wakiwa kazini, kundi la wezi lilivamia ofisi aliyokuwa akilinda. Walikuwa zaidi ya watano, na kabla hajajua kinachoendelea walimrukia kwa nguvu. Walimfunga mikono yake kwa kamba na kumziba mdomo kwa kitambaa ili asiweze kutoa kelele. Macho yake yalishuhudia wezi hao wakibeba vitu vyote vya thamani ofisini ile – kompyuta, fedha na nyaraka muhimu – huku yeye akiwa hana la kufanya.
Alikaa pale sakafuni kwa masaa kadhaa hadi alfajiri, ndipo alipofanikiwa kujisogeza na kuomba msaada. Lakini kilichomshangaza ni kwamba kesho yake, alipomwendea bosi wake kueleza kilichotokea, hakupata masikio ya huruma. Badala yake, bosi alimwambia kwa ukali:
“Wewe Mzee Juma, lazima ulipanga njama na hao wezi. Nani asiyekuwa mjinga kiasi cha kuacha mali ya kampuni iende ovyo hivyo?” Soma zaidi hapa

Post a Comment