Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema vijana wake wako tayari kutetea Ngao ya Jamii pale watakapochuana na watani zao Simba katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho
Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Folz alisema mechi hiyo haitakuwa na tofauti na mechi nyingine walizocheza kitu pekee kitakachoongezeka ni kucheza mbele ya mashabiki wengi na watahakikisha wanashinda mchezo huo ili kuwapa furaha mashabiki wao
"Tuna shauku kuelekea mchezo huu, ni mechi kubwa ya kukaribisha msimu, tutahakikisha tunacheza vyema na katika utaratibu wetu bila ya kujali tunacheza na nani"
"Itakuwa mechi kubwa mbele ya mashabiki wengi, tutahakikisha tunawapa mashabiki wetu furaha na kutetea Ngao ya Jamii kwa msimu mwingine," alisema Folz
Folz ameongeza kuwa katika mchezo huo, mashabiki watarajie mabadiliko makubwa kuanzia upangaji wa kikosi aina yao ya uchezaji
"Tumecheza na kupata matokeo mazuri katika mechi za kirafiki lakini mchezo wa kesho tutakuwa tofauti kwa sababu hii ni mechi ya ubingwa. Hivyo tutarajie kuiona Yanga yenye utofauti kuanzia upangaji wa kikosi na uchezaji"
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au Bonyeza HApa Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

Post a Comment