Kocha mkuu wa Yanga afunguka haya kuelekea mechi yao ya kesho dhidi ya Mbeya City


 Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Sokoine

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mkoani Mbeya mapema leo, Folz alisema ameiandaa timu yake kucheza katika mazingira yoyote

Amesema timu bora inakuwa tayari kubadilika kufuatana na mazingira, wataonyesha ubora wao katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soko mkoani Mbeya

"Timu Bora inakuwa tayari kucheza katika mazingira yeyote , haijalishi pitch ni mbaya kiasi gani tutacheza kwa ubora wetu na tutabadilika kulingana na mazingira," alisema Folz

Katika hatua nyingine Folz amewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kuwaunga mkono katika kazi wanayoifanya. Folz amesema wamekusudia kuifikisha Yanga katika sehemu ambayo haijawahi kufika, wanachohitaji ni muda na uungwaji mkono wa kila mmoja

"Tunataka kuifikisha Yanga hatua ambayo haijawahi kufika kwenye mashindano ya kimataifa, huu ni mchakato na tunaendelea kutengeneza timu taratibu. Kitu nina uhakika nacho tutafika mbali mahali ambapo hatujawahi kufika," aliongeza Folz

Yanga ilitua Mbeya jana ambapo leo itakamilisha maandalizi yake katika uwanja wa Sokoine ambao utatumika siku ya kesho

Usikose kuitazama mechi hii LIVE kupitia Simu yako pia ukiwa na app hii utaweza kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post