Visa vya wizi wa magari vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali katika nchi jirani. Kila wiki kuna habari moja au mbili zikihusu wizi wa gari, jambo ambalo awali sikulipa uzito nikiamini huenda ni uvumi tu.
Lakini majuzi nilikumbana na tukio la moja kwa moja baada ya gari langu aina ya Harrier kuibwa katikati mwa jiji la Nairobi. Visa hivi kwa kawaida huripotiwa katika vituo vya Polisi lakini bila mafanikio, kwani mara nyingi maafisa wa usalama huahidi kuwakamata wahusika ila kufikia sasa hakuna matokeo.
Rafiki yangu mmoja naye aliwahi kupokonywa gari akiwa barabara kuu ya Thika na majambazi waliokuwa na bunduki. Alipeleka taarifa katika kituo cha Polisi cha Kamukunji lakini hadi leo hakuna aliyekamatwa wala gari kurejeshwa. Hali hii ilinifanya kuwa mwangalifu zaidi kwani kazi yangu ya Taxi ndiyo tegemeo langu kuu. Kupitia kazi hiyo nimeweza kuwalipia karo watoto wangu na kuhudumia familia yangu. Soma zaidi hapa

Post a Comment