Katika kijiji kimoja kilicho nje kidogo ya mji wa Morogoro, aliishi binti mmoja aliyeitwa Agnes, mwenye umri wa miaka ishirini na nane. Agnes alikuwa binti mpole, mwenye bidii na heshima kubwa kwa wazazi wake. Alifanya kazi ya biashara ndogondogo sokoni na kwa juhudi zake ndizo zilizomsaidia kujikimu kimaisha na pia kuwasaidia wazazi wake.
Miaka michache nyuma, Agnes alikutana na kijana mmoja aitwaye George, ambaye alimvutia sana. George alikuwa mzuri kwa maneno, mwenye ucheshi na aliweza kumfanya Agnes ahisi kama ndiye mwanamke pekee ulimwenguni. Walipoanza uhusiano, Agnes alijitolea kwa dhati kumpenda na kumjali. Ndoto yake kubwa ilikuwa kuolewa na George, na walipokuwa wakizungumza, George alimwambia wazi kwamba alitaka kumuoa lakini hana pesa za mahari.
Kwa kuwa moyo wa Agnes ulikuwa umejaa mapenzi, aliamua kumsaidia. Kwa miezi kadhaa aliweka akiba yake yote, akiuza baadhi ya mali ndogo ndogo alizokuwa nazo, na hatimaye akafanikiwa kukusanya zaidi ya milioni kumi. Kwa imani kubwa na bila hofu, alimkabidhi George pesa hizo akidhani zitatumika kulipia mahari nyumbani kwao. Machozi ya furaha yalimbubujika alipompa, akihisi sasa ndoto yake ya ndoa iko karibu kutimia. Soma zaidi hapa

Post a Comment