Wakati kiungo Khalid Aucho akiwa tayari anajifua na kikosi cha Singida Black Stars, walima alizeti hao pia wamekamilisha usajili wa wachezaji wengine watatu walioitumikia Yanga msimu uliopita
Mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage amekamilisha uhamisho wa kutua Singida BS jana akisaini mkataba wa mwaka mmoja
Kibabage alikuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na Yanga lakini makubaliano ya pande mbili yamefikiwa na sasa anajiunga na Singida BS kwa uhamisho wa moja kwa moja na sio mkopo tena
Lakini pia Singida BS imewasajili viungo Jonas Mkude na Clatous Chama ambao wote walikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu uliopita
Nyota hao wanaungana na kocha Miguel Gamondi ambaye aliongoza Yanga kwa takribani mwaka mmoja na nusu kabla ya kupewa mkono wa kwaheri msimu uliopita
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.
.jpeg)
Post a Comment