Katika kijiji kimoja kilichopo pembezoni mwa mji wa Mwanza, aliishi mwanamke kijana aliyejulikana kwa jina la Mercy. Mercy alikuwa ameolewa na mume wake aitwaye Joseph kwa kipindi cha takribani miaka minne. Ndoa yao ilianza kwa furaha tele, lakini kadiri muda ulivyopita, changamoto moja kubwa ilianza kujitokeza—kutopata mtoto.
Katika jamii yao, mtoto huonekana kama nguzo ya ndoa na baraka ya kifamilia. Mercy alijaribu kwa kila njia kuhakikisha anapata ujauzito: alitembelea hospitali mbalimbali, alitumia dawa za hospitali, hata akajitahidi kuzingatia lishe bora kama alivyoelekezwa na madaktari. Lakini kila mara vipimo vilionyesha hali ya kawaida, jambo lililomchanganya sana.
Miaka ilivyokuwa ikisonga, maumivu yake yaliongezeka. Joseph, mume wake, alianza kulalamika mara kwa mara. Alikuwa akimwambia:
“Mercy, tumekaa muda mrefu bila mtoto. Familia yangu inaniona kama mimi si kitu. Nifanyeje sasa?”
aneno hayo yalimuumiza sana Mercy. Kila mara alijiona kama mzigo katika ndoa yake. Jirani zake nao walimnong’oneza nyuma ya mgongo wake, wakimcheka na kumuita “mwanamke tasa.” Hali hii ilimfanya akose furaha, akawa anakaa kimya mara nyingi na kulia peke yake usiku. Soma zaidi hapa

Post a Comment