Jina langu ni Miriam kutoka Mombasa. Nilikuwa kwenye uhusiano wa miaka minne na mwanaume niliyempenda kwa dhati. Tulipitia mengi pamoja, tukaanza maisha kwa shida, tukilala kwenye chumba kimoja cha kupanga bila hata kitanda cha maana.
Nilijitahidi kuwa nguzo ya maisha yake, nikimfariji kila aliposhindwa na kumtia moyo kila alipoonekana kukata tamaa. Nilidhani mapenzi yetu yangedumu maisha yote. Lakini siku moja mambo yalibadilika ghafla.
Baada ya kupata ajira ndogo jijini, alianza kubadilika taratibu. Aliendelea kujifanya yuko bize, simu zangu akawa hapokei tena kama zamani, na mawasiliano yetu yakawa ya mbali sana. Nilianza kuhisi kuna kitu si cha kawaida.
Haikuchukua muda mrefu kabla ya kusikia tetesi kwamba amepata mwanamke mwingine, tajiri na mwenye uwezo mkubwa kifedha. Nilipojaribu kumkabili kwa upole, hakunificha chochote.
Aliniambia wazi kwamba maisha yangu hayakuwa kiwango chake tena. Nilihisi kama moyo wangu umepasuka vipande vidogo. Nilijaribu kujishawishi kwamba maisha yataendelea, lakini ukweli ni kwamba nilikuwa nimeumia kupita maelezo. Somz zaidi hapa

Post a Comment