Simba kukipiga na Gor mahia SIMBA DAY

Ni rasmi, klabu ya Simba imethibitisha wababe wa soka la Kenya klabu ya Gor Mahia, itapamba Tamasha kubwa zaidi la burudani ukanda wa Afrika Mashariki na kati, SIMBA DAY

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema wameialika Gor Mahia katika tamasha hilo litakalofanyika Septemba 10 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

"Tumeialika Gor Mahia katika Tamasha letu la Simba Day, tumekuwa na changamoto ya kupata timu kutokana na ratiba ilivyokaa, ligi tayari zimeshaanza na timu nyingi ziko kwenye mashindano"

"Lakini hatimaye tumeipata timu ya Gor Mahia ambayo ni timu kongwe pale Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla"

"Gor Mahia ni timu yenye mashabiki wengi pale Kenya hivyo kuwaalika kwenye Tamasha hili pia tunatanua wigo wetu katka ukanda huu," alisema Ahmed

Kikosi cha Simba tayari kimerejea nchini wakitokea Misri baada ya kukamilisha wiki nne za pre-season

Simba itakuwa na takribani wiki moja kukamilisha maandalizi yake kuelekea Tamasha hilo

Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post