Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili mshambuliaji Suleiman Mwalimu Gomez kutoka Wydad Athletic
Mwalimu aliyezitumikia Singida BS/Fountain Gate kabla ya kutimkia Wydad, anarudi Tanzania kwa mkopo wa msimu mzima Simba ikiwa na nafasi ya kumsajili moja kwa moja pale muda wa mkopo utakapomalizika
Ni usajili uliokuwa ukisubiri uthibitisho tu kwani Simba ilikamilisha usajili wake tangu wiki iliyopita na alitua nchini juzi tayari kuungana na waajiri wake wapya
Mwalimu aliitumikia Wydad katika michuano ya kombe la Dunia la klabu mwezi Juni akipata nafasi katika mechi zote tatu mojawapo ikiwa dhidi ya Manchester City
Kuelekea msimu ujao safu ya ushambuliaji ya Simba sasa itaongozwa na Jonathan Sowah, Mwalimu na Steven Mukwala baada ya Lionel Ateba kuuzwa
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

Post a Comment