Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepitia na kufanya marekebisho muhimu ya kanuni zitakazotumika kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26. Maboresho haya yamelenga kuongeza ushindani, uwajibikaji, na ubora wa ligi. Hapa tumekuandalia muhtasari wa mabadiliko makuu:
1. Kanuni ya 62 – Wachezaji wa Kigeni (Kipengele 1.2)
Klabu hairuhusiwi kusajili zaidi ya golikipa mmoja wa kigeni kwa mashindano yote yaliyo chini ya TFF. Hatua hii inalenga kudhibiti ubora na usawa wa ligi kwa kuhakikisha nafasi ya mlinda mlango inapewa kipaumbele kwa vipaji vya ndani.
2. Kanuni ya 39 – Waamuzi (Kipengele 7.1)
Kamati ya Waamuzi ya TFF sasa inaweza kupanga waamuzi kutoka nje ya Tanzania kusimamia michezo ya Ligi Kuu ya NBC. Lengo ni kuongeza uwajibikaji na ubora wa uchezeshaji kwa kuleta waamuzi wenye uzoefu wa kimataifa.
3. Kanuni ya 41 – Udhibiti wa Wachezaji
Mchezaji atakayepokea kadi ya njano kwenye michezo minne (4) hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu yake. Awali, adhabu hii ilitolewa baada ya kadi tatu pekee. Sasa imesogezwa hadi nne, ikiongeza nidhamu na kuwapa wachezaji nafasi ya kucheza kwa uwangalifu zaidi.
4. Kanuni ya 08 – Mshindi (Bingwa)
Endapo timu zitamaliza zikiwa na pointi sawa, bingwa atapatikana kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo kwa mpangilio:
Matokeo ya moja kwa moja baina ya timu husika (Head to Head).
Tofauti ya magoli.
Idadi ya magoli yaliyofungwa.
Idadi ya mabao yaliyofungwa dhidi.
Ushindi wa michezo ya ugenini mingi zaidi.
5. Kanuni ya 17 – Taratibu za Mchezo
Timu zinaruhusiwa kutumia vyumba vya kuvalia (Dressing Rooms) saa 8 kabla ya mchezo kuanza.Timu itakayoshindwa kutekeleza kanuni hii itafungiwa kutumia uwanja wake wa nyumbani kwa michezo isiyopungua mitatu.
Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

Post a Comment