Aisha alikuwa mfanyabiashara mdogo jijini Mombasa, akiuza nguo na viatu sokoni. Alipoanza biashara yake, kila kitu kilionekana kuenda vizuri.
Wateja walikuwa wanamiminika dukani kwake, na ndani ya mwaka mmoja alifungua tawi la pili. Marafiki zake walimwona kama mfano wa kuigwa, na kila mtu alisema angekuwa mfanyabiashara mkubwa wa baadaye.
Lakini maisha yanaweza kubadilika ghafla. Mambo yalianza kuharibika kidogo kidogo. Wateja wake wakawa wanapungua bila sababu inayoeleweka.
Gharama ya kodi ya duka ilipanda, na mara kwa mara alipata hasara kubwa. Marafiki waliokuwa karibu naye walianza kumsema nyuma ya pazia, wengine wakimcheka kwamba alijifanyia maamuzi makubwa kuliko uwezo wake.
Ndani ya miezi michache tu, Aisha alipoteza mtaji wake wote. Maduka yake mawili yakafungwa, na akabaki akihangaika kulipa madeni. Aliporudi sokoni, alijikuta hana hata ka-meza ya kuuza bidhaa ndogo ndogo. Kila kitu alichokuwa amejenga kwa miaka mingi kiliporomoka kwa macho yake. Soma zaidi hapa

Post a Comment