Avamiwa na mbu wote wa mtaa baada ya kuiba mume wa rafiki yake

 

Asubuhi ya Jumamosi, wakazi wa mtaa wa Nguvumali, Tanga, walishuhudia tukio la ajabu na la kutatanisha lililowaacha midomo wazi. Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Halima, alijikuta akishambuliwa na kundi kubwa la mbu waliomvaa kwa wingi kiasi cha kushindwa hata kupumua vizuri, tukio lililozua tafrani na taharuki mitaani.

Wakazi walidai kuwa Halima alionekana akikimbia ovyo barabarani akipiga mayowe, huku akijipiga na kujikuna kila mahali mwilini akidai kuwa mbu walikuwa wakimvamia kwa makusudi.

Watu waliokuwa jirani walijaribu kumsaidia kwa kumpaka dawa ya mbu na kumfunika na blanketi, lakini hakuna kilichofua dafu—mbu walizidi kujaa na kumzingira, tofauti kabisa na hali ya kawaida.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa Halima alikuwa akihusishwa na skendo ya kuvunja ndoa ya rafiki yake wa karibu aitwaye Amina, ambaye kwa muda mrefu alikua akimwamini kama dada. 

Inadaiwa kuwa Halima alianza uhusiano wa siri na mume wa Amina, na hata baada ya ukweli kugundulika, hakuonyesha majuto yoyote bali aliendelea kuishi na mwanaume huyo kama mke wa pili kwa kificho. Soma zaidi hapa 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post