Ally kamwe awastukia Simba asema Dabi ya ngao ya Jamii isihairishwe


 Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Simba una umuhimu wa kipekee kwani fedha zitakazopatikana zitakwenda kusaidia yatima na wale wenye uhitaji

Kamwe amesema mchezo huo unapaswa kupigwa kama ulivyopangwa Septemba 16 lakini kama kuna ulazima wa kuchezwa mapema Yanga iko tayari mchezo huo kupigwa siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi Septemba 12

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu mchezo huo zikiibuka taarifa kuwa klabu ya Simba imeomba usogezwe mbele kwa kuwa Septemba 20 wanakabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali nchini Botswana

Kamwe amebainisha kuwa Yanga haina tatizo na tarehe ya mchezo huo na wako tayari kucheza lakini kama italazimu, urudishwe nyuma Septemba 12 ili kuondoa 'kipengele'

"Mchezo wa Ngao ya Jamii una umuhimu mkubwa sana kwani mapato yatakayopatikana yanakwenda kusaidia Jamii hivyo sisi (Yanga) tuko tayari kucheza katika tarehe hiyo iliyopangwa"

"Hata sisi tuna mchezo Angola lakini naamini muda uliopo utatosha kwa timu kusafiri na kukamilisha maandalizi kwani Angola na Botswana sio mbali ni mwendo wa saa chache tu"

"Lakini kama haiwezekani, sisi tuna mchezo wa wiki ya Mwananchi Septemba 12 na tutacheza dhidi ya Bandari Fc. Tuko tayari kuwa 'stopisha' Bandari Fc ili mchezo upigwe siku hiyo," alisema Kamwe

Usikose kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post