Mpaka sasa inaelezwa Simba imekamilisha usajili wa nyota watano wa kigeni katika mkakati wa kukiboresha kikosi cha Simba kuelekea mikiki mikiki ya michuano mbalimbali msimu ujao
Katika orodha hiyo kuna mawinga wawili, beki wa kushoto, kiungo mkabaji na mshambuliaji mmoja
Winga Mofosse Tresor Karidioula kutoka klabu ya Haras El Hodood ya Misri anatajwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba katika dirisha hili
Beki wa kushoto Khadim Diaw kutoka klabu ya Al Hilal ya Sudan nae tayari amemalizana na Simba kama ilivyo kwa kiungo mkabaji Alassane Kante kutoka klabu ya CA Bizertin ya Tunisia
Lakini pia yumo winga Mohammed Bajaber anayetua Msimbazi akitokea klabu ya Polisi ya Kenya huku pia mshambuliaji Jonathan Sowah akitajwa tayari kamalizana na Simba akitokea klabu ya Singida Black Stars
Mlinda lango Yacoub Mohamed kutoka klabu ya JKT Tanzania anaongoza wachezaji wa ndani ambao tayari wamemalizana na Simba kama ilivyo kwa beki wa kati Wilson Nangu ambaye pia anatokea JKT Tanzania
Kiungo kutoka Coastal Union Hussein Semfuko nae ametajwa kuwa tayari amemalizana na Wekundu hao wa Msimbazi
Tetesi bado zinaihusisha Simba na nyota kadhaa wa kigeni na ndani kama kiungo wa Zoman Fc, Privat Djessan Bi, Feisal Salum - Azam Fc, Yahya Zayd - Azam Fc, Abdallah Kulandana - Fountain Gate na mshambuliaji Dramane Kamagate anayeitumikia San Pedro ya Ivory Coast
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema wamekamilisha usajili wa nyota wote waliowahitaji katika dirisha hili lakini zoezi la usajili litafungwa baada ya kumalizika michuano ya CHAN 2024 itakayoanza kutimua vumbi August 02 hadi Augut 30 katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania
Ahmed alisema watatumia michuano hiyo kumalizia nafasi chache ambazo wataziacha mahsusi wakiamini kuna nafasi ya kupata wachezaji bora katika michuano hiyo
Semaji ametamba kuwa Simba itakapoanza kutambulisha wachezaji, wengine wote watakaa kimya kwa mshtuko watakao-kutana nao
Usikose kuitazama mechi ya YANGA VS SAFARI LAGER CUP LIVE bure kupitia simu yako download App yetu kutazama mechi hii bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure Bonyeza Hapa kudownload App yetu bure kumbuka kuidownload kama Apk maana bado haijawekwa playstore
.jpeg)
Post a Comment