Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure
Idownload kwa kubonyeza HAPA au HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha
Mlinzi mahiri wa kulia wa Klabu ya Yanga, Yao Kouassi, amerudi nchini mapema huku akiwa na ari na hamasa mpya kuelekea maandalizi ya msimu wa mashindano wa 2025/26.
Nyota huyo raia wa Ivory Coast amerejea akiwa na dhamira ya kujiandaa kikamilifu kwa kurejea dimbani baada ya kipindi cha kuuguza jeraha.
Yao alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi Mei, kufuatia majeraha ya muda mrefu yaliyokuwa yakimkabili na kumuweka nje ya uwanja mara kwa mara.
Upasuaji huo ulifanyika nchini Tunisia, hatua muhimu iliyowezesha mwanzo mpya katika safari ya kurejea kwake uwanjani.
Awali, taarifa zilieleza kuwa beki huyo angekuwa nje kwa takriban miezi sita, lakini habari njema ni kwamba maendeleo yake ni ya kutia moyo. Tayari amekamilisha awamu ya kwanza ya matibabu na sasa ameanza mazoezi mepesi akiwa na morali ya juu, jambo linaloashiria uwezekano wa kurejea mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Hata hivyo, Yanga italazimika kuwa na subira zaidi kidogo kabla ya kumpokea rasmi uwanjani, kwani bado anahitaji muda wa kuimarika na kurudi katika hali yake kamili ya ushindani.
Beki huyo aliyepata mapokea mazuri kutoka kwa mashabiki tangu alipojiunga na Yanga, ameonesha kujitoa kwa dhati na kupambana kuhakikisha anarudi kwa kiwango bora zaidi.
Bila shaka urejeo wake utakuwa ni faida kubwa kwa safu ya ulinzi ya timu hiyo katika msimu ujao.
Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

Post a Comment