RASMI: Yanga wajitoa kwenye kinyanganyiro cha kumsajili Fei Toto wawaachia Simba

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu hiyo imekamilisha michakato yote ya usajili katika dirisha hili, kazi wanayoendelea nayo ni kuwatambulisha wachezaji wapya na wale walioongeza mikataba kabla ya mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwenda pre-season

Kauli hiyo inamaliza rasmi tetesi zilizokuwa zinawahusisha baadhi ya wachezaji akiwemo kiungo wa Azam Fc Feisal Salum 'Fei Toto'

Aidha Kamwe amethibitisha kuwa jezi namba 6 ambayo zamani aliitumia Feisal kabla ya kuchukuliwa na Skudu Makudubela, imepata mtu mwingine

"Sisi tumefunga michakato yetu ya usajili hivyo nikuhakikishie Feisal Salum hatasajiliwa na Yanga"

"Jezi namba 6 haikutumika mwaka jana lakini msimu ujao itatumika kwani tayari imepata mtu," alisema Kamwe

Mpaka sasa Yanga imetambulisha usajili wa nyota wanne wapya ambao Moussa Balla Conte(DM), Abdulnasir Mohammed 'Casemiro' (DM), Offen Chikola (AM) na Lassine Kouma (CAM)

Wachezaji wengine wanaosubiri utambulisho Yanga ni pamoja Aboubakar Nidhar Otham (CB), Celestin Ecua (AM), Mohamed Doumbia (CM), Mohammed Hussein (LB) na Andy Boyeli (CF)

Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs SAFARI LAGER CUP Live bure kupitia app yetu bonyeza hapa kuidownload sasa pia ukiwa na app hii utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure download sasa

Kutazama chanel za Azam tv bure kwa wale mnaotumia App ya Phoenix angalia juu kwenye hii post kisha bonyeza neno Read original


Follow page yetu👉🏻👉🏻 Kwa habari za michezo zaidi bofya hapa


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post