JS KABYLIE WAANZA MAZUNGUMZO YA KUMG'OA JEAN CHARLES AHOUA SIMBA

JS KABILYE WAANZA MAZUNGUMZO YA KUMG'OA JEAN CHARLES AHOUA SIMBA

Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure

Idownload kwa kbonyeza HAPA au HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha


 Klabu ya JS Kabylie ya Algeria imewasilisha ofa rasmi kwa Simba SC wakimtaka kiungo mshambuliaji nyota Jean Charles Ahoua, ambaye aling’ara kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/25.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba, klabu hiyo ya Algeria imeonyesha nia ya dhati ya kumnasa Ahoua, aliyehusika moja kwa moja katika mabao 25 ya Simba msimu uliopita, akifunga 16 na kutoa asisti 9.

Hata hivyo, Ahoua bado ana mkataba wa miaka miwili na Simba, na hivyo uamuzi wa kuuzwa au kubaki uko mikononi mwa Wekundu hao wa Msimbazi.

Simba walimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita, lakini waliandika historia kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup), Ahoua akiwa sehemu muhimu ya mafanikio hayo kwa kufunga mabao manne katika mashindano hayo na kuchaguliwa kwenye kikosi bora cha msimu cha CAF.

Wakati hayo yakiendelea, Simba wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutoka Azam FC. Feisal alikuwa kinara wa asisti kwenye Ligi Kuu msimu uliopita akiwa na jumla ya pasi 14 za mabao, akionyesha ubunifu na uthubutu mkubwa kwenye eneo la mwisho.

Hata hivyo, kocha wa Simba, Fadlu Davids, anaripotiwa kutopendelea kumuachia Ahoua katika dirisha hili la usajili, akimtaja kama mchezaji muhimu kwenye mfumo wake kuelekea msimu wa 2025/26.

Usikose kuzitazama mechi hizi leo ARSENAL vs NEW CASTLE, TANZANIA vs SENEGAL na BARCELONA vs VISSEL KOBE  LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post