ELIE MPANZU BADO YUPO YUPO SANA SIMBA HII HAPA TAARIFA KAMILI
Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure
Idownload kwa kbonyeza HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha
Kiungo mshambuliaji wa Simba Elie Mpanzu ni miongoni mwa wachezaji waliorejea jijini Dar es salaam kutoka mapumzikoni ili kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2025-2026
Mpanzu ameungana na nyota wengine ambao walianza kuwasili mapema wiki hii tayari kwa pre-season hiyo ambayo itakuwa Misri
Nyota huyo raia wa DR Congo aliyejiunga na Simba kupitia dirisha dogo la msimu uliopita na kuhusika katika mabao 10, akifunga manne na kuasisti sita alikuwa akitajwa huenda asingerejea
Mpanzu amemaliza tetesi hizo zilizokuwepo karibu wiki nzima zikidai ana mgogoro wa mkataba aliokuwa nao Simba na klabu iliyokuwa inammiliki
Simba haikuwa tayari kumpoteza nyota wake huyo muhimu ambapo inaelezwa klabu iliweka utaratibu maalum wa kumpatia ulinzi alipotoka DR Congo hadi kufika jijini Dar es salaam
"Huu ni utaratibu ulioanzishwa kwa siku za karibuni na Simba kwa nia ya kuwalinda wachezaji kutokana hizi hila za baadhi ya timu kuwabeba wachezaji wanahusishwa na klabu yetu. Sio Mpanzu tu, kila mchezaji hata wale wapya wamwekuwa wakiwekewa ulinzi mara wanapowasili," alisema mtoa taarifa
Usikose kuitazama mechi ya LIVERPOOL VS YOKOHAMA live bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuitazama mechi hii live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure Bonyeza hapa kudownload
Au
.jpeg)
Post a Comment