Azam Fc wafunguka usajili wa Fei toto kwenda Simba
Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure
Idownload kwa kubonyeza HAPA au HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Azam FC, Thabit Zacharia maarufu kama Zakazakazi, amefunguka kuhusu sababu zinazowazuia kumuuza kiungo mshambuliaji Feisal Salum Fei Toto kwa klabu ya Simba SC.
Kupitia mahojiano maalum, Zakazakazi amesema wazi kuwa Azam FC haiwezi kumuuza mchezaji huyo kwa Simba kutokana na kipengele maalum kilichopo kwenye mkataba wao na klabu ya Yanga, walipomnunua mchezaji huyo awali.
"Hatuwezi kumuuza Feisal kwenda Simba kwa sababu sidhani kama Simba wana pesa za kuweza kumnunua Feisal," amesema.
Zakazakazi ameweka wazi kuwa wakati Azam FC ilipomsajili Feisal kutoka Yanga SC, walikubaliana kuwa endapo mchezaji huyo atauzwa kwa Simba, basi Azam italazimika kuilipa Yanga fidia ya shilingi bilioni moja za Kitanzania.
"Wakati tunamchukua Feisal kutoka Yanga, yapo makubaliano ya kimkataba kuwa endapo tutamuuza mchezaji huyo kwa klabu ya Simba, tunapaswa kuilipa Yanga Tsh Bilioni 1," alifichua.
Ameongeza kuwa ili kufanikisha uhamisho huo, Simba italazimika kutoa dau kubwa litakalowezesha Azam kupata faida zaidi ya fidia hiyo, jambo ambalo linaonekana kuwa gumu.
"Sasa Simba watalipa shilingi ngapi tufanye biashara? Sisi hatuko tayari kulipa Bilioni 1 kwa Yanga kama dau lao litakuwa dogo, na pia lazima walipe dau ambalo litatufanya tupate zaidi ya Yanga," alisisitiza.
Pamoja na mijadala mingi inayoendelea mitandaoni kuhusu tetesi za uhamisho wa Fei Toto kwenda Simba, Zakazakazi amesema hadi sasa hawajapokea ofa yoyote rasmi kutoka kwa Simba.
Yanga ndio ilikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kumrejesha Feisal, hata hivyo Wananchi wameachana na mpango huo baada ya kukamilisha usajili wa kiungo mshmbuliaji Lassine Kouma ambaye ni mahiri zaidi katika nafasi ya namba 10
Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

Post a Comment