Aucho na Yanga ndo basi tena Aamua kuondoka


 Kiungo wa Yanga Khalid Aucho
huenda asiwe sehemu ya kikosi
cha mabingwa hao wa kihistoria
msimu ujao baada ya
majadiliano ya kuhuisha mkataba
wake kutofikia mwafaka,
imefahamika

Yanga ilikuwa tayari kumpa
Aucho mkataba wa mwaka
mmoja lakini kiungo huyo
hayuko tayari kuongeza mwaka
mmoja, akihitaji mkataba wa
miaka miwili

Mtu wa karibu wa Aucho ambaye
ni mwanahabari, amesema
Aucho huenda akaelekea
Vietnam alikopata ofa nono zaidi

"Baada ya kikao cha wiki nzima,
mimi kama Mwanahabari
niliyekuwa na nafasi ya
kuyaongea kutoka kwake na
uongozi wa Yanga, rasmi Aucho
hatokuwa na Yanga"

"Aucho anaweza kwenda
Vietnam, kuna klabu ya Ligi Kuu
ya huko imemuhitaji, naweza
kusema Aucho hatakuwepo
nchini msimu ujao," alisema

Awali Yanga ilikuwa na
makubaliano na Aucho
kumuongeza mkataba wa mwaka
mmoja lakini huenda fundi huyo
kutoka Jinja akawa amebadili
mawazo baada ya kushawishiwa
na ofa kutoka nje

Katika eneo analocheza Aucho,
Yanga tayari imemsajili kiungo
Mohamed Doumbia huku pia
ikihusishwa kukamilisha usajili
wa kiungo kutoka CS Sfaxien
Moussa Balla Conte

Huna sababu ya kukosa kutazama michuano ya CHAN LIVE kupitia Simu yako

Michuano hii itaanza Agosti 02, kwa mechi ya ufunguzi kuchezwa katika dimba la Benjamin Mkapa kwa wenyeji Taifa Stars kucheza dhidi ya Burkina Faso.

Usikose kuitazama michuano hii LIVE  bure kupitia simu yako  download App hii mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi pia App bado hatujaiweka playstore hivo italeta neno This file might be harmful usiogope


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post