Ilikuwa ni siku ya kawaida katika mtaa wa Kihonda mjini Morogoro, lakini haikuwahi kuwapo siku kama hiyo kabla. Kliniki moja ya mtaa, inayojulikana kwa jina la “Afya Njema”, ilivamiwa na wananchi wenye hasira baada ya taarifa za kushangaza kuibuka kwamba mganga wake mkuu alikuwa akiwawekea wagonjwa wake damu ya mbuzi kwenye dawa zao na kuwaambia ni “dozi maalum ya kinga ya ndani.”
Kwa muda mrefu, kliniki hiyo ilikuwa maarufu kwa kuwasaidia wagonjwa wenye maradhi ya muda mrefu, hasa wale waliokata tamaa hospitali kubwa. Wagonjwa walielekea hapo kwa matumaini makubwa, wengi wao wakielezwa “wana tatizo la damu” na kupewa juisi ya giza giza isiyojulikana, wakidaiwa ni dawa ya kuongeza seli nyekundu. Soma zaidi hapa.
Post a Comment