Klabu ya Zamalek ya Misri imeongeza kasi ya harakati zake za kumsajili mshambuliaji tegemeo wa Yanga SC, Clement Mzize, kwa kuongeza dau lao la awali ambalo lilikataliwa na mabosi wa klabu hiyo ya Tanzania.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na uongozi wa Yanga, Zamalek tayari imetuma ofa mpya ya takribani dola 750,000 za Kimarekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2 za Kitanzania, ikiwa ni jitihada mpya ya kuhakikisha wanamnasa Mzize kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Awali, Yanga ilipokea ofa ya chini kutoka kwa Zamalek, lakini ilikataliwa kwa kuwa haikufikia matarajio ya klabu hiyo ambayo ipo kwenye harakati za kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu na kombe la CRDB. Hata hivyo, ongezeko la dau limefungua milango ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili.
Mbali na Zamalek, inadaiwa kuwa Yanga pia imepokea ofa kutoka klabu ya JS Kabylie ya Algeria na Al-Ittihad ya Libya, lakini hakuna hata moja iliyofanikiwa kuwashawishi viongozi wa Yanga kama ilivyofanya Zamalek.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, kuna kila dalili kwamba Mzize atatua Zamalek, huku usajili wake ukitarajiwa kuiingizia Yanga kitita kizito cha fedha ambacho kitasaidia katika mipango ya maboresho ya kikosi chao.
Ni dhahiri kuwa Yanga imeanza kuingia sokoni kufanya biashara ya wachezaji wake nyota, jambo lililoonekana wazi baada ya kumuuza kiungo wake nyota Stephane Aziz Ki kwa Wydad Athletic ya Morocco kwa ada ya karibu Tsh Bilioni 2.
Mlinda mlango namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra, naye anatajwa kuwa katika rada za klabu mbalimbali, huku taarifa zikieleza kuwa Yanga imepokea ofa za kuvutia kutoka nje ya nchi.
Yanga inaonekana kuwa katika mpango wa kuongeza mapato kupitia mauzo ya baadhi ya wachezaji, huku ikijiandaa kufanya usajili wa maboresho kuelekea msimu ujao wa mashindano ya ndani na kimataifa.
Usikose kuitazama mechi hii ya SIMBA SC vs SINGIDA BS LIVE bure kupitia simu yako download App hii mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi pia App bado hatujaiweka playstore hivo italeta neno This file might be harmful usiogope
Au hapa chini
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)
- Wezesha “Unknown Sources” kwenye setting ya Simu yako. Nenda kwenye “Settings” > “Security” au “Privacy“.
Post a Comment