Klabu ya Yanga SC imeanza harakati rasmi za kuinasa saini ya kiungo wa chini kutoka Djoliba AC ya Mali, Daba Benoit Diakite, mwenye umri wa miaka 21.
Kiungo huyu chipukizi anayetokea Afrika Magharibi kwa sasa ndiye bidhaa inayowindwa na wengi, na Yanga wameingia kwenye vita ya kusaka huduma yake, wakimtazama kama mrithi sahihi wa Khalid Aucho ambaye umri unamtupa mkono
Diakite ameibuka kuwa mmoja wa viungo wa chini wanaopigiwa hesabu zaidi Afrika kufuatia msimu bora na Djoliba. Licha ya umri wake mdogo, ameonesha ukomavu wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kuwasoma wapinzani, kuzuia mashambulizi, pamoja na kupiga pasi za kujenga mashambulizi. Hii imewafanya vigogo wa Afrika na Ulaya kumvizia kwa karibu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mali, Diakite amebakiza mkataba wa mwezi mmoja tu na Djoliba, jambo linalomfanya awe mchezaji huru kuanzia mwezi ujao. Hili limewavutia sana Yanga ambao wamekuwa makini katika kuimarisha safu ya kiungo kufuatia kuondoka au kupungua kwa kiwango cha baadhi ya wachezaji wao wa eneo hilo.
Diakite si mchezaji wa kawaida. Klabu kubwa kama Manchester United waliwahi kutuma mpelelezi wao (scout) kumfuatilia moja kwa moja, huku Benfica ya Ureno nao wakionesha nia ya kumchukua. Barani Afrika, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Esperance de Tunis ya Tunisia nao wanawania saini yake. Kwa hali hii, Yanga wanakabiliwa na ushindani mkali.
Kiungo huyo ameweka wazi kwamba anataka kipengele maalum kwenye mkataba wake na Yanga iwapo atasajiliwa – kipengele cha kumruhusu kuondoka haraka pindi atakapopata ofa kutoka Ulaya. Hii inaonyesha kuwa Diakite ana ndoto za kucheza soka la juu barani Ulaya, na Yanga wanapaswa kumshawishi kwa mipango bora ya maendeleo ya mchezaji.
Kwa mujibu wa duru za ndani, wakala wa Diakite ana uhusiano mzuri na uongozi wa Yanga. Kwa miaka ya karibuni, tayari amehusika kuwasajili wachezaji wanne tofauti waliotua Jangwani. Hili linaipa Yanga faida ya mazungumzo na nafasi ya kuifanikisha dili hii haraka kuliko wapinzani wao.
Je Yanga watamvuta Diakite kutoka midomoni mwa vigogo wa Afrika na Ulaya? Kama wakifanikiwa, basi bila shaka watakuwa wamepata hazina mpya ya kiungo wa chini, ambaye si tu ataimarisha timu kwa sasa, bali pia anaweza kuwa mali ya kuuza kwa faida kubwa siku za usoni
Au hapa chini
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)
- Wezesha “Unknown Sources” kwenye setting ya Simu yako. Nenda kwenye “Settings” > “Security” au “Privacy“.
Post a Comment