Kwa miaka mingi, nilimshuhudia ndugu yangu John akizama kwenye dimbwi la pombe. Alianza kwa kileo cha kawaida, lakini kadri siku zilivyopita, pombe ikawa sehemu ya maisha yake ya kila siku.
Mwanzoni, tulidhani ni msongo wa maisha, labda matatizo ya kazini au mambo ya familia, lakini baadaye ikawa wazi kuwa hali yake ilikuwa mbaya zaidi. Alianza kupoteza kazi moja baada ya nyingine, na hatimaye, mke wake alimwacha, akaondoka na watoto.
Siku moja nilimpata amekaa kwenye kibaraza cha nyumba ya jirani akiwa hana viatu, suruali yake ikiwa imechanika, na harufu ya pombe ikitoka mwilini mwake kama jasho. Macho yake yalikuwa mekundu, na maneno aliyokuwa akitamka hayakuwa na maana.
Nililia kimoyomoyo. Huyu si yule kaka yangu niliyekua...SOMA ZAIDI
Post a Comment