Nilikuwa nimeota mara nyingi kuwa mama. Kila nilipoona mwanamke akibeba mtoto mchanga, moyo wangu ulijaa hamu isiyoelezeka. Niliolewa nikiwa na miaka 27, na baada ya miezi kadhaa ya ndoa, niligundua kuwa nilikuwa mjamzito.
Furaha yangu haikuwa na kifani. Nilimwambia mume wangu tukiwa mezani usiku mmoja na machozi ya furaha yakinitiririka. Aliinuka, akanikumbatia na kusema, “Hatimaye! Tutakuwa wazazi!”
Lakini furaha hiyo haikudumu. Nilipoenda kliniki ya kwanza baada ya wiki kadhaa, daktari aliniangalia na kusema kwa sauti ya chini, “Samahani, hatuoni mapigo ya moyo ya mtoto.” Nilihisi dunia ikizunguka.
Nilikuwa na mimba ya miezi miwili na nusu tu, na tayari ilikuwa imeharibika. Nililia kwa siku nyingi, lakini mume wangu alikuwa...SOMA ZAIDI
Post a Comment