Yanga yapania rekodi nyingine Azam Complex
Ni Jumapili ya kufosi pale uwanja wa Azam Complex, Chamazi siku ya Jumapili katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Yanga imedhamiria kushinda mchezo wa kwanza nyumbani baada ya ushindi katika mechi mbili za ugenini
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kuhakikisha wananunua tiketi mapema lengo likiwa kujaza dimba la Azam Complex
Tangu msimu uliopita, Yanga ilichagua uwanja wa Azam Complex kama sehemu ya machinjio ya timu pinzani na kilichotokea ni kuwa Yanga ilishinda mechi zote 13 iliyozocheza katika uwanja huo
Aidha Yanga iliweka rekodi ya kibabe msimu uliopita kwani ilishinda mechi zote 15 ilizocheza nyumbani
Msako wa rekodi nyingine unaanza Jumapili dhidi ya KMC ambayo imepata wakati mgumu kila ilipokutana na Yanga
Msimu uliopita KMC walibugizwa mabao 5-0 katika mchezo dhidi ya Wananchi hapo Chamazi
Msimu huu wanakuwa timu ya kwanza kukutana na Yanga katika uwanja wa nyumbani
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment