Mo afurahishwa na 'mzuka' Simba
Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, amewapongeza wachezaji wa Simba baada ya kuiuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex jana
Mo ameeleza kufurahishwa na ari, morali iliyoonyeshwa na wachezaji katika mchezo huo ulioihakikishia Simba ushindi wa tatu mfululizo kwenye ligi
"Ushindi dhidi ya Azam Fc! Hongera kwa wachezaji wetu kwa kujituma na kuonyesha moyo wa ushindi. Tutaendelea kujenga safari yetu ya mafanikio," aliandka Mo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Mabao ya Lionel Ateba na Fabrice Ngoma yaliihakikishia Simba ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya Azam Fc na kusogea mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi
Unaweza kusema matunda ya uwekezaji wa Mo katika kikosi cha Simba msimu huu yameanza kuonekana, kikosi cha kocha Fadlu Davids kikionyesha mabadiliko makubwa kiuchezaji
Mo ametumia takribani Bilioni 8 kuisuka upya Simba katika dirisha lililopita la usajili
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment