Yanga imebaki na wachezaji 11 tu
Katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA, Yanga imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Kiluvya Fc na Cosmopolitan Fc ambapo wananchi wameshinda mechi zote
Waliichapa Kiluvvy Fc mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Septemba 04 mabao ya Salum Abubakar, Jean Baleke na Shekhan Khamis
Jana Yanga ikapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cosmopolitan yote yakifungwa na Maxi Nzengeli
Kutokana na kukosa idadi kubwa ya wachezaji wake, kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ametumia utaratibu wa kucheza mechi hizo ili kuwaweka nyota wake katika hali ya ushindani kwani hakuna maandalizi ya kimbinu ambayo atafanya wakati huu anawakosa wachezaji 16
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema ni wachezaji 11 tu waliobaki kambini wakiendelea na maandalizi
"Tumesajili wachezaji 27, kati yao 14 wako katika majukumu ya timu za Taifa na wawili ni majeruhi"
"Hivyo tuna wachezaji 11 tu kambini na tumelazimika kuwaongeza wachezaji kutoka timu ya vijana," alisema Kamwe
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment