Taarifa Mpya kutoka yanga ni kuhusu Yao Kouassi
Bado unahangaika kutafuta app ya kutazama mechi za ligi kuu tz bara (nbc premier league) pia na mechi za ulaya? Basi hii hapa app itakayokuwezesha kutazama mechi zote Live bure kabisa pia ndani ya app hii utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure kudownload app hii bonyeza 👉🏻HAPA
Baada ya kukosekana uwanjani kwa wiki kadhaa, mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi amerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa raundi ya pili ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA ya Ethiopia
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi ijayo, Septemba 14 katika uwanja wa Abebe Bikila, Adis Ababa
Yao aaliumia mazoezini wakati wakijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar
Kwa sasa Mlinzi huyo wa kulia ameanza mazoezi makali chini ya kocha wa Viungo Taibi Lagrouni, ambaye ndiye anayesimamia mpango mzima wa kusimamia utimamu wake
Yanga itavaana na CBE baada ya kila moja kuvuka raundi ya kwanza ya michuano hiyo, vijana wa Gamondi wakiing'oa kwa kishindo Vital'O ya Burundi kwa ushindi wa mabao 10-0, huku Wahabeshi wakiitoa SC Villa ya Uganda kwa mabao 2-1
No comments:
Post a Comment