Kwa sasa akili ya Simba iko katika michuano ya kombe la Shirikisho (CAF CC) ambapo Mnyama anahitaji kuiondosha Al Ahly Tripoli na kutinga hatua ya makundi
Ni mechi mbili muhimu za kuamua hatma ya michuano hiyo ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Septemba 15 huko Libya na mechi ya marudiano kupigwa Septemba 22 jijini Dar es salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya kumalizana na Al Ahly Tripoli, Simba itarejea katika mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC ambapo Mnyama atakabiliwa na mechi nyingine mbili za kukamilisha mwezi Septemba
Mzizima Dabi ndio itakayofuata, Septemba 26 Simba ikichuana na Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na kisha Mnyama kusafiri mkoani Dodoma/Manyara kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo mwingine wa ligi kuu utakaopigwa Septemba 29
Simba imeanza vyema ligi kwa kushinda mechi mbili za mwanzo na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali ametamba kuwa Mnyama hana mpango wa kuondoka kileleni mpaka 'kieleweke!'
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment