Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema watahakikisha wanapambana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ken Gold hapo kesho ili kupata ushindi utakaoendelea kuweka vyema malengo yao katika mbio za ubingwa msimu huu
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo, Gamondi alisema anatambua mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu kila timu inayocheza na Yanga hujipanga kusaka matokeo mazuri dhidi yao
Hata hivyo amesema ubora wa kikosi chake unampa matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya
"Ni mchezo wetu wa pili kwenye ligi kuu, bado kuna safari ndefu lakini huu ni mchezo muhimu kwetu na tunahitaji kupata matokeo. Leo jioni kwenye mazoezi ya mwisho nitaona Uwanja kama utaturuhusu kucheza mchezo wetu basi itakuwa nzuri kwa upande wetu na kama itakuwa tofauti tutahakikisha tunapambana kupata ushindi"
"Siku zote timu yoyote ikicheza na Yanga wanakuwa makini na kutafuta matokeo kama sisi, tutacheza kwa tahadhari na tuna wachezaji wazuri wenye uzoefu wa kucheza kwenye mazingira yoyote"
"Najua mashabiki wetu wanapenda tushinde magoli mengi, lakini sisi kama walimu tunaangalia sana kwenye uhalisia na kitu cha muhimu kwetu ni ushindi na kama mechi itaturuhusu tupate magoli mengi basi tunajituma mpaka mwisho kufanya hivyo, "alisema Gamondi
Kikosi cha Yanga kilitua mkoani Mbeya jana na leo watafanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa Sokoine
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment