Baada ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa ushindi wa kibabe wa jumla ya mabao 7-0 dhidi ya CBE SA ya Ethiopia, kikosi cha Yanga kinahamishia nguvu zake katika ligi kuu ya NBC
Yanga inaelekea mkoani Mbeya tayari kwa mchezo dhidi ya Ken Gold utakaopigwa Jumatano, Septemba 25 katika uwanja wa Sokoine
Wananchi wakitoka Mbeya, watarejea Dar es salaam kucheza mechi yao ya kwanza nyumbani msimu huu dhidi ya KMC katika uwanja wa Azam Complex, Septemba 29
Baada ya KMC, Wananchi watabaki nyumbani kuikaribisha Mashujaa Fc katika mchezo mwingine utakaopigwa uwanja wa Azam Complex
Katika mchezo dhidi ya CBE juzi, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alifanya mabadiliko ya kikosi chake katika baadhi ya nafasi ambapo baada ya mchezo alidokeza kuwa mabadiliko hayo yalizingatia ratiba ya mechi mfululizo za ligi itakayofuata
Yanga inashika inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ikiwa imecheza mechi moja tu ambayo ni dhidi ya Kagera Sugar wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment