Huu ni msimu wa furaha Msimbazi - Ahmed
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema kuwa wachezaji wote waliopo ndani ya kikosi cha Simba msimu huu wapo tayari kupambania uzi wa Unyamani kuwapa furaha Wanasimba
Baada ya mismu mitatu ya kukosa taji la ligi kuu huku msimu uliopita Mnyama akikosa nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Afrika, Ahmed amesema maboresho makubwa ya kikosi yaliyofanyika katika dirisha hili la usajili, yatakwenda kurejesha heshima ya Simba msimu huu
Baada ya kuhitimisha Simba Day kwa kishindo ambapo Mnyama aliinyoa APR kwa mabao 2-0, Ahmed amesema sasa wanakwenda kukaribisha msimu August 08 dhidi ya watani zao Yanga na wanamsimbazi watarajie kuona Simba nyingine kabisa
"Wachezaji wote wa Simba wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25 na tunatambua kwamba msimu uliopita haukuwa mzuri kwetu kutokana na kushindwa kufikia malengo yetu"
"Lakini tunaanza upya kuyakimbiza malengo yetu, msimu huu tunasema ni Ubaya, Ubwela tutaanza na Ngao ya Jamii," alitamba Ahmed
Simba ilirejea mazoezini jana baada ya mapumziko ya siku moja ambapo kikosi kinakamilisha maandalizi ya mwisho kabla ya kuikabili Yanga katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii siku ya Alhamisi
Simba ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambapo lengo ni kuhakikisha Ngao inaendelea kusalia Msimbazi kwa msimu mwingine
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment