Chama afurahia mwanzo mzuri Yanga
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Clatous Chama amefurahia mwanzo mzuri na Wananchi juzi akiwa sehemu ya kikosi kilichohitimisha wiki ya Mwananchi kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Red Arrows ya Zambia
Chama alitua Yanga katika dirisha hili la usajili akitokea klabu ya Simba ambayo pengine keshokutwa atashuka dimbani kuikabili katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
"Tumepata mechi nzuri katika wiki ya Mwananchi na maandalizi mazuri ya pre-season kwa kucheza mechi za Kimataifa"
"Nafurahi tumeshinda na kufunga Tamasha la Wiki ya Mwananchi kwa furaha. Hongera kwa umoja wa timu na tutarajie ushindi zaidi," aliandika Chama katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Chama ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kufanya mambo makubwa katika kikosi cha Yanga msimu huu
Wale wanaompima kupitia mechi hizi za pre-season wasimalize maneno, wasubiri kumuona katika mechi za mashindano
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment