Mo apiga hodi Azam Fc kumtaka Fei Toto - EDUSPORTSTZ

Latest

Mo apiga hodi Azam Fc kumtaka Fei Toto

Mo apiga hodi Azam Fc kumtaka Fei Toto

Michuano ya EURO 2024 inaendelea pia ligi mbali mbali karibu zinaanza usikose kuzitazama mechi hizi zote LIVE bure kupitia simu yako download app yetu kutazama chanel zote za Azam tv bure pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili download app yetu sasa kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA

Azam FC's attacking midfielder Feisal Salum

Photo: Courtesy of Azam FC
Azam FC's attacking midfielder Feisal Salum

Klabu ya Simba imefungua mazungumzo na Azam Fc kwa ajili ya kumtaka kiungo mshambuliaji Feisal Salum 'Fei Toto', imefahamika

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba, imethibitisha kuwa tayari mabosi wa Simba na Azam Fc wamekutana mara mbili na kuna matumaini ya makubaliano kufikiwa

Simba ina makubaliano binafsi na Fei Toto kuhusu maslahi yake, kilichokuwa kimebaki ni makubaliano baina ya klabu juu ya ada ya uhamisho

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ameuwekea kipaumbele usajili wa Fei Toto kwani anaamini mchezaji huyo ataongeza ubora kwenye eneo la kiungo cha ushambuliaji hasa baada ya Clatous Chama kuondoka

Azam Fc wamekuwa 'wazito' kumuachia Fei Toto kwa kuwa nao watashiriki michuano ya Kimataifa (Ligi ya Mabingwa) msimu ujao lakini tajiri 'Mo' ameonyesha utayari wa kununua mkataba wa Fei ili kuhakikisha anatua Msimbazi

Fei Toto alimaliza msimu uliopita akiwa kinara wa mabao katika kikosi cha Azam Fc akifunga mabao 19 na kutoa assist 7

Msimu wake mmoja na Azam Fc umetosha kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi kwa mchezaji wa Azam Fc katika msimu mmojaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz