Kuna Aziz Ki, Chama, Pacome na Maxi
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga jana walitangaza kumsajili kiungo mshambuliaji Clatous Chama aliyeng'olewa kutoka kwa watani zao Simba
Usajili huo ni wazi unakwenda kuongeza upana wa kikosi hasa katika eneo la viungo washambuliaji ambao sasa ni jukumu la kocha Miguel Gamondi kuamua nani aanze kwenye kikosi
Kabla ya kusajiliwa kwa Chama, Gamondi amekuwa na nyota watatu aliowategemea zaidi kama viungo wa ushambuliaji ambao ni Max Nzengeli, Aziz Ki na Pacome Zouzoua ambao msimu uliopita walifunga jumla ya mabao 39
Usajili huo wa Chama ndani ya Yanga sasa utamfanya kocha Gamondi kuwa na machaguo mengi zaidi katika eneo hilo ingawa Mzambia huyo pia ana uwezo wa kucheza kama mshambuliaji anayetokea pembeni kama ilivyo kwa Pacome na Maxi
Katika msimu wake wa mwisho na Simba, Chama alipachika mabao saba na pia akitokea assist 7
Chama amejiunga na Yanga baada ya tetesi za muda mrefu, Mzambia huyo alimaliza mkataba wake wa kuichezea Simba Juni 30, mwaka huu
Haikuwa rahisi kwake kufikia uamuzi wa kujiunga na Yanga kwani klabu yake ya zamani Simba walikuwa tayari kumbakisha kwa gharama yoyote
Hadi mapema jana alipotambulishwa, viongozi wa Simba walikuwa bado wanahaha wakijaribu kumshawishi asitishe mpango wa kutua Jangwani
Post a Comment