Try Again awataja walioisaliti Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Try Again awataja walioisaliti Simba

Try Again awataja walioisaliti Simba

Leo ndio leo ni ZAMBIA vs TANZANIA usikose kuitazama mechi hii live kabisa bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree pia ndani ya app hii kuna muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili na chanel za azam tv na Dstv bofya sasa kuidownload bure

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah 'Try Again' amejiuzulu nafasi hiyo na kumuomba mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji 'Mo' kurudi kuiongoza.

Try Again amefikia uamuzi huo baada ya kuhudumu kwenye uongozi ndani ya Simba kwa takribani miaka saba ambapo minne alikuwa Mwenyekiti wa muda wa Klabu na mitatu Mwenyekiti wa kuteuliwa na Bodi ya Simba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Try Again amesema amekaa na Mwekezaji wa Simba, MO na kumpa ripoti ya klabu hiyo wapi wamefeli msimu uliomalizika na nini wanatamani kukifanya ili timu hiyo iweze kusonga mbele.

"Kuiokoa Simba na kuitoa katika nafasi iliyopo sasa ni Mo pekee ambaye anaweza kufanya hivyo kwa kuitoa ilipo sasa na kuipeleka mbele, nimekuwa nikizungumza naye mara kwa mara hadi mara kumi lengo ni kuona anarudi kuijenga Simba imara na bora," alisema na kuongeza;

"Nimefanya mazungumzpo naye na kumuomba arudi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, mimi nitabaki kuwa mwanachama na nitakuwa kiongozi ambaye nitakuwa tayari kuitumikia Simba wakati wowote."

Try Again alisema yeye ni mwanachama na kiongozi wa timu hiyo, ni mdogo kuliko klabu, hivyo ameamua kuachia nafasi hiyo ili kumuachia kiongozi ambaye anamuamini na anaamini ataipeleka Simba kwenye mafanikio.

"Mashabiki, wanachama wa Simba wanataka mafanikio na hata sisi viongozi tunatamani hayo mafanikio na tunaumia mara mia ya mashabiki kwa sababu sisi tunafanya uwekezaji na tunataka matokeo mazuri ili tupate sifa kutoka kwa mashabiki na wanachama, hakuna kiongozi ambaye anafurahia timu kushuka kimafanikio," alisema na kuongeza;

"Viongozi waliobaki wanatakiwa kupewa ushirikiano, nawaomba mashabiki kuondokana na migogoro ili kumpa uwanda mpana mwekezaji kuongoza timu kwa mafanikio bila kusikia minong'ono kutoka kwa wanachama na mashabiki wa timu, kiongozi hatakiwi kuongoza timu yenye migogoro."


WACHEZAJI WASALITI KUNG'OKA SIMBA

Wakati huohuo, Try Again amefunguka kuwa pamoja na Simba kutajwa kuwa ni timu mbovu msimu uliomalizika, wao kama viongozi wamebaini wachezaji virusi ndani ya timu ambao amekiri hawatakuwa na nafasi msimu ujao.

"Simba hii inayotajwa kuwa ni mbovu msimu huu ikicheza na Ihefu FC unaiona kweli inapata shida kuonyesha ushindani lakini hiyohiyo ndio inafanya vizuri ikikutana na Al Ahly hivyo kutokana na hilo tumegundua kuwa kuna vitu ambavyo sio sawa vilikuwa vinafanya na wachezaji.

"Kuna wachezaji kwenye kikosi chetu ni wasaliti hawatakuwa na nafasi msimu ujao kwa sababu tumegundua ndio waliotuangusha pia kuna wachezaji ambao tuliwasajili tukiamini watakuja kutupa matokeo lakini mambo yamekuwa tofauti, hili halianzii Simba tu bali timu nyingi wanakutana na changamoto hiyo, tumesajili wachezaji zaidi ya watano kama Fabrice Ngoma, Che Malone, wamefanya kazi nzuri, Luis Miquisson licha ya kutokuwa bora lakini kapata nafasi," alisema.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA CHUMBANIDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz