TETESI Za Usajili Simba SC 2024/2025 - EDUSPORTSTZ

Latest

TETESI Za Usajili Simba SC 2024/2025

Klabu ya Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 24 kwaajili ya kuipata huduma yake Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.

Joyce Lomalisa Simba SC

Joyce Lomalisa Simba SC

Mbali na Nouma, Simba pia awali ilitajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki, Joyce Lomalisa aliyemaliza mkataba ndani ya Yanga ambapo timu hiyo inaangalia uwezekano wa kumpata beki wa kushoto aende kusaidiana na Mohamed Hussein.

Salum Athuman ‘Stopper’ Simba SC

Salum Athuman ‘Stopper’ Simba SC

Klabu ya Simba inajaribu kufanya mazungumzo ya kumsajili beki wa KVZ ya Zanzibar, Salum Athuman ‘Stopper’ ambaye amekuwa na kiwango bora.

Yannick Bangala Azam FC

Yannick Bangala Azam FC

Viongozi wa Simba wametajwa kufanya mawasiliano na wakala wa kiungo, Yannick Bangala anayeichezea Azam FC ili kuangalia uwezekano wa kumpata nyota huyo wa zamani ya Young Africans.

Brian Mandela Onyango Simba SC

Brian Mandela Onyango Simba SC

Klabu ya Simba inamuwania beki wa kati wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini raua wa Kenya, Brian Mandela Onyango mwenye miaka 29.

Samwel Onditi Simba SC

Samwel Onditi Simba SC

Klabu ya Simba imefanya mawasiliano na wawakilishi beki, Samwel Onditi wa Geita Gold, kwaajili ya Kuangalia uwezekano wa kumsajili beki huyo mwenye uwezo wa Kucheza kama beki na kiungo wa kati ambaye kwa sasa ni mchezaji huru

Steve Komphela Simba SC

Steve Komphela Simba SC

Klabu ya Simba ipo kwenye Mazungumzo ya mwisho na Kocha Steve Komphela mwenye umri wa miaka 56 kutoka Afrika Kusini ili arithi mikoba ya iliyoachwa na Kocha Abdelhack Benchikha.

Serge Pokou Simba SC

Serge Pokou Simba SC

Klabu ya Simba inatajwa kuwa Katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo, Serge Pokou mwenye umri wa miaka 23 kutoka ASEC Mimosas ya kwao Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh200mil.

Kenneth Semakula Simba SC

Kenneth Semakula Simba SC

Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na aliyekuwa kiungo wa SC Villa ya Uganda, Kenneth Semakula ili kujiunga nao msimu ujao.

Derrick Mukombozi Simba SC

Derrick Mukombozi Simba SC

Uongozi wa Simba SC upo kwenye mazungumza ya kunasa saini na beki wa Namungo na timu ya taifa ya Burundi, Derrick Mukombozi kwaajili ya kuziba pengo la Henock Inonga ambaye anatajwa kutaka kuondoka klabuni hapo.

Elie Mpanzu Simba SC

Elie Mpanzu Simba SC

Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano ya kumsajili winga wa kulia wa kimataifa wa DR Congo na klabu ya AS Vita Club, Elie Mpanzu mwenye umri wa miaka 22 kwa Mkataba wa miaka miwili.

TETESI Za Usajili Simba SC 2024/2025, Tetesi Za Usajili Simba Dirisha Kubwa la Usajili 2024/2025, Usajili Simba 2024,Tetesi za Usajili Simba Dirisha Kubwa, Tetesi za Usajili Simba Leo,Tetesi za Usajili Tanzania,Usajili simba dirisha kubwa, Mwanaspoti tetesi za usajili leo,Usajili simba mwanaspoti,Tetesi za Usajili Simba SC Dirisha Kubwa la usajili 2024.

Inaelezwa kuwa Klabu ya Simba SC ipo kwenye mipango ya kumsajili Mshambuliaji, Agostinho Cristóvão Paciência maarufu ‘Mabululu’ raia wa Angola kutoka Al Ittihad Alexandria ya Misri.

Mabululu mwenye umri wa miaka 31 amefunga magoli jumla ya mabao 10 kwenye mechi 16 za Egyptian Premier League msimu huu.

Ousmane Fernandez Drame Simba SC, Mohamed Damaro Camara Simba SC.Klabu ya Simba imetajwa kuwa ipo mbioni kuwasajili Wachezaji wawili wa Hafia FC ya Guinea, Mohamed Damaro Camara mwenye miaka 21 na Ousmane Fernandez ‘Drame’ mwenye umri wa miaka 23.

Wachezaji hao wanatajwa kuja kuchukua nafasi ya Sadio Kanoute anayedaiwa kuomba kuondoka mwishoni mwa msimu pamoja na Fabrice Ngoma.

Usajili huo umetajwa ni kwaajili ya kuimarisha eneo la kiungo, ambapo Camara anacheza nafasi ya kiungo mkabaji, huku Drame akiwa na uwezo wa kucheza namba sita pamoja na namba nane.

Fiston Kalala Mayele Simba SC

Fiston Kalala Mayele Simba SC

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ Kupitia A-fm Radio amesema kuwa wametuma maombi kwenye Klabu ya Pyramids FC ya nchini Misri ya kumpata Kwa Mkopo aliyekuwa Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele.

Klabu ya Simba imefikia Makubaliano ya kumnunua beki wa kati, Lameck Lawi kutoka Klabu yake ya Coastal Union ya Tanga.

Uongozi wa klabu ya Simba umepanga kupiga hodi kwenye klabu ya Azam kwaajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ayoub Lyanga, imefahamika.

Mkataba wa Lyanga na Azam unafikia mwishoni mwa msimu huu na tayari mabosi wa Azam wameanzisha mazungumzo ya kumuongezea mkataba licha ya Simba nao kuweka dau lao mezani kwa nyota huyo.

Yusuph Kagoma Simba SC

Yusuph Kagoma Simba SC

Kiungo, Yusuph Kagoma yupo mbioni kujiunga na klabu Simba SC akiwa Mchezaji huru baada ya kuachana na Singida Fountain Gate FC.

Pa Omar Jobe Simba SC

Pa Omar Jobe Simba SC

Klabu ya Simba huenda ikaachana mshambuliaji wake, Pa Omar Jobe mazungumzo yanakaribia kukamilika.

Saido Ntibanzonkiza Simba SC

Saido Ntibanzonkiza Simba SC

Kiungo wa klabu ya Simba SC, Saido Ntibanzokinza raia wa Burundi ameachana rasmi na Klabu hiyo.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz