Klabu za Dodoma Jiji, Mashujaa na JKT Tanzania zinapigana vikumbo kuiwania saini ya Nassoro Kapama ambaye amemaliza mkataba wake wa miezi sita na Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja.
Klabu za Kagera Sugar, KMC FC, Coastal Union na Dodoma Jiji, zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya kiungo wa Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja, Juma Nyangi.
Klabu za Singida Fountain Gate, Pamba Jiji na Singida Black Stars zimeingia Katika vita ya kuwania saini ya beki wa Tabora United, Andy Bikoko raia wa DR Congo.
Klabu za Simba Queens na Yanga Princess zimeingia kwenye vita ya kumuwinda beki wa kati wa Alliance Girls, Anita Adongo ambaye anamaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.
Klabu ya Ceasiaa Queens inatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazohitaji huduma ya Kiungo wa Alliance Girls, Nelly Kache.
Klabu ya Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 24 kwaajili ya kuipata huduma yake Kuelekea Msimu Mpya wa 2024/2025.
Aliyekuwa Mshambuliaji wa Simba, Mkongomani, Jean Othos Baleke yupo nchini akiwa katika mazungumzo na timu mbili ambazo ni Azam FC na Young Africans
Inaelezwa kuwa Baleke aliyecheza Simba kwa mkopo akitokea TP Mazembe ya kwao DR Congo kabla ya kutimkia Al Ittihad ya Libya mwaka huu, yupo nchini kwaajili ya kukamilisha usajili wa kujiunga na kati ya Azam FC au Young Africans.
Klabu ya Pamba Jiji ya Jijini Mwanza iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2024/2025 inaendelea kuboresha kikosi chake na sasa imetua kwa Mshambuliaji wa Ken Gold, Edgar Wiliams aliyeibuka kinara wa ufungaji kwenye Championship.
Klabu ya Singida Black Stars inadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na Mshambuliaji Victorien Adebayo kutoka AS GNN ya kwako Nigeria pamoja na golikipa, Mohamed Kamara kutoka AC Horoya ya Guinea.
Adebayor aliyewahi kucheza RS Berkane na AmaZulu kabla ya kurejea kwao Niger anaitajika haraka ili kuziba nafasi ya Emmanuel Bola Labota anayetakiwa Young Africans.
Klabu ya Azam FC imedaiwa kuwa kwenye hatua nzuri ya kumuongezea mkataba mpya winga wake, Ayoub Lyanga ili asalie kikosini hapo.
Golikipa wa Klabu ya Yanga, Aboutwalib Mshery amemaliza mkataba wake na Klabu hiyo, wakati akisubiria hatma yake klabu ya Azam imetajwa Kuanza Mazungumzo naye.
Baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia Azam FC, beki Edward Charles Manyama ametajwa kuwaniwa Al Hilal ya Sudan na muda wowote anatatajiwa Kusaini Mkataba Mpya.
Klabu ya Dodoma Jiji imetajwa kuwa Katika hatua za mwisho kumsajili, Meck Mexime kwaajili ya kuchukuwa nafasi ya Francis Baraza aliyeachana na timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika
Mexime atajiunga na Dodoma Jiji baada ya kuachana na Singida Black Stars zamani Ihefu Fc.
Klabu za Simba Queens, Yanga Princess pamoja na Police Bullets ya Kenya zimepiga hodi kunako Fountain Gate Princess kuiwania saini ya kiungo Mkenya Involata Mukoshi ambaye anamaliza mkataba Msimu huu.
Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Athuman Masumbuko amepanga kuachana na timu hiyo baada ya kutokuwa na msimu mzuri msimu ulioisha wa 2023/2024.
Uongozi wa Singida Black Stars umeingilia kati dili la kiungo wa Tabora United, Najim Mussa ambaye ametajwa kuwaniwa na timu mbalimbali zikiwemo za Simba SC na Azam FC.
Klabu ya Simba Queens imeanza mazungumzo ya kumnunua moja kwa moja winga wa JKT Queens, Winifrida Gerald anayemaliza mkataba mwishoni mwa mwezi huu.
Klabu ya Azam FC imeanza Mazungumzo na Klabu ya Zesco ya Zambia ili kuona uwezekano wa kumpata kipa, Ian Otieno kwaajili ya kuchukua nafasi ya Mohamed Mustafa aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Al-Merrikh ya kwao Sudan ambaye hawana uhakika wa kusajilia klabuni hapo.
Golikipa Hussein Masalanga rasmi ameachana na Ihefu Fc baada ya mkataba wake kutamatika ndani ya klabu hiyo.
Kiungo wa klabu ya Simba SC, Saido Ntibanzokinza raia wa Burundi ameachana rasmi na Klabu hiyo.
Klabu ya Azam Fc imeachana na beki wake Malickou Ndoye, Azam pia inatarajiwa kuachana na Abdulai Idrisu, Issah ndala pamoja na Ali Ahmada.
Klabu ya Yanga sc imepanga kuwaongeza mikataba mipya wachezaji Salum Abubakar, Jonas Mkude, Bakari Nondo Mwamnyeto pamoja na Kibwana Shomari.
Mchezaji Cheikh Sidibe ameomba kuondoka ndani ya Klabu ya Azam Fc.
Golikipa wa klabu ya Azam FC, Mohamed Mustapha atarejea kwenye klabu yake ya Al Mereikh dirisha lijalo la Usajili baada ya mkopo wa miezi 6 kuisha.
Klabu ya Pamba Jiji iliyopanda Ligi Kuu ipo mbioni kumsajili aliyewahi kuwa Kocha wa Vilabu vya Simba SC na Tabora United, Goran Kopunovic.
Kiungo, Yusuph Kagoma yupo mbioni kujiunga na klabu Simba SC akiwa Mchezaji huru baada ya kuachana na Singida Fountain Gate FC.
Klabu ya Simba inajaribu kufanya mazungumzo ya kumsajili beki wa KVZ ya Zanzibar, Salum Athuman ‘Stopper’ ambaye amekuwa na kiwango bora.
Klabu ya Simba inamuwania beki wa kati wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini raia wa Kenya, Brian Mandela Onyango mwenye miaka 29.
Klabu ya Mashujaa FC imetajwa Kuanza Mazungumzo na aliyekuwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Seif Abdallah Karihe ili kuziba nafasi ya Adam Adam aliyerejea Azam FC.
Viongozi wa Simba wametajwa kufanya mawasiliano na wakala wa kiungo, Yannick Bangala anayeichezea Azam FC ili kuangalia uwezekano wa kumpata nyota huyo wa zamani ya Young Africans.
Klabu ya Azam FC imetajwa kuanza mazungumzo ya kumrejesha winga wa zamani wa timu hiyo, Farid Mussa aliyemaliza mkataba huko Young Africans.
Golikipa Yona Amosi yupo huru baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya timu yake ya Tanzania Prisons FC.
Klabu ya Simba huenda ikaachana mshambuliaji wake, Pa Omar Jobe mazungumzo yanakaribia kukamilika.
Klabu ya Mashujaa ipo kwenye mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya golikipa wake, Erick Johora.
Kipa huyo wa zamani wa vilabu vya Eagle Noir na Yanga sc alijiunga na Mashujaa Kwa mkataba wa miezi 6 akitokea Geita Gold
Klabu ya Dodoma Jiji imetajwa kutuma ofa ya kuhitaji golikipa, Sebu Sebu baada mkataba wake kumalizika ndani ya klabu ya Geita Gold.
Vilabu vya KMC FC, Kengold, na Tanzania Prisons vinaiwania Saini ya beki Geofrey Muha baada ya mkataba wake na Geita Gold kumalizika.
Uongozi wa Simba SC upo kwenye mazungumza ya kunasa saini na beki wa Namungo na timu ya taifa ya Burundi, Derrick Mukombozi kwaajili ya kuziba pengo la Henock Inonga ambaye anatajwa kutaka kuondoka klabuni hapo.
Klabu ya Yanga Princess imeanza maandalizi mapema ya msimu ujao baada ya kumfuata kiungo wa JKT Queens, Amina Bilal ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Kuna uwezekano mkubwa wa beki wa kushoto, Deusdedith Okoyo akajiunga na Pamba Jiji ya Jijini Mwanza iliyopanda daraja msimu huu.
Klabu ya JKT Tanzania imeanza hesabu za usajili wa winga wa Kagera Sugar FC, Richaldson Ng’odya.
Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na aliyekuwa kiungo wa SC Villa ya Uganda, Kenneth Semakula ili kujiunga nao msimu ujao.
Klabu ya Coastal Union imeanza hesabu za kumnasa beki wa Simba, Kennedy Juma baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu.
Hiyo inatokana na kuondokewa na beki wa kikosi hicho, Lameck Lawi ambaye tayari msimu ujao atajiunga na Simba baada ya kufikia makubalino baina ya timu hizo na kusainishwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu ya Singida Black Stars, inawania saini ya kiungo mshambuliaji wa Gor Mahia, Austin Odhiambo kwaajili ya kujiunga nao msimu ujao.
Taarifa zinaeleza nyota wawili wa Kenya, Elvis Rupia na Duke Abuya ndio ambao wanatumika kama chambo cha kumshawishi kiungo huyo japo changamoto kubwa inayoweza kutokea ni kutokana na Gor Mahia kufuzu Ligi ya Mabingwa.
Kiungo Mshambuliaji, Saidi Zanda yupo huru baada ya mkataba wake na klabu ya Stand United ya mkoani shinyanga inayoshiriki Championship kumalizika.
Baada ya kuitumikia Namungo Kwa takribani misimu mitano (5) mfululizo Hashimu Manyanya yupo huru baada ya mkataba wake kutamatika mwishoni mwa msimu uliopita.
Taarifa ambazo Nijuze Habari inazo hadi Sasa hakuna mazungumzo yaliyofanyika kuhusu kuongezewa mkataba mpya na klabu hiyo.
Yusuph Valentino Mhilu yupo huru baada ya mkataba wake na Geita Gold kutamatika tangu May 2024.
Muhilu amekulia Kwenye timu ya vijana ya Yanga Sc, pia amewahi itumukia Kagera Sugar Kwa nyakati tofauti
Mashambuliaji wa Zamani wa TP Mazembe ya DR Congo, Eliud Ambokile ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya klabu ya Mbeya City inayoshiriki Championship.
Golikipa, Mohamedi Hussein maarufu kwa jina la Mudi Colour yupo huru baada kumaliza mkataba wake na Dodoma Jiji FC ya Dodoma.
Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji na Tanzania Prisons, Salum Kihimbwa ni mchezaji huru.
Beki wa Geita Gold, Erick Kyaruzi maarufu Mopa amemaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo hivyo yupo huru.
Mkataba wa Haruna Kassim Shabani maarufu Tiote na Mtibwa Sugar umemalizika na Sasa ni mchezaji huru.
Post a Comment