Coastal Union iko kwenye mazungumzo na beki wa zamani wa Klabu ya Yanga, Djuma Shaaban.
Mkongomani huyo amekuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima bila ya kuwa na timu baada ya kuachana na Yanga aliyoitumikia kwa misimu miwili 2021-2022 na 2022-2023.
Inaelezwa kwamba jana alielekea Tanga kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Coastal ambao wanaimarisha kikosi chao kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Shirikisho msimu ujao.
Post a Comment