Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kuanza Julai 06 na kumalizika Julai 22 jijini Dar es salaam na Zanzibar
Taarifa iliyotolewa CECAFA imebainisha kuwa michuano hiyo imerudishwa nyuma ili kwendana na kalenda ya mashindano ya CAF inayotarajiwa kuanza mwezi August
Aidha klabu za TP Mazembe (DR Congo), Red Arrows (Zambia) na Nyasa Big Bullets (Malawi) zimethibitisha kushiriki baada mwaliko wa CECAFA
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambao ni Yanga, Azam fc iliyoshika nafasi ya pili, Simba na Coastal Union zilizoshika nafasi ya tatu na nne ni miongoni mwa klabu zitakazoshiriki michuano hiyo inayorejea baada ya kutofanyika kwa misimu miwili
Timu nyingine ni Vital 'O, APR FC, El Merreikh, Al Hilal, Hai El Wadi, Gor Mahia FC, SC Villa, JKU SC na El Merreikh FC-Bentiu
BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA UJIFUNZE MAUTUNDU YA CHUMBANI
No comments:
Post a Comment