Simba yamtaka kiungo Mganda, Kennedy Juma... hizi hapa tetesi za usajili ligi kuu tz bara leo jumatatu - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba yamtaka kiungo Mganda, Kennedy Juma... hizi hapa tetesi za usajili ligi kuu tz bara leo jumatatu

Simba yamtaka kiungo Mganda, Kennedy Juma...

Leo ni ENGLAND vs BOSNIA pia GERMANY vs UKRAINE usikose kuzitazama mechi hizi live buree kwenye simu yako pia kutakuwa na mechi kati ya TANZANIA vs ZAMBIA bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hizi live kabisa bureee pia ukiwa na app hii utaweza kutazama chanel zote za azam tv na Dstv na muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili bofya sasa kuidownload pia yale mambo yetu yale yapo

Klabu ya Simba iko kwenye mazungumzo ya kumpata aliyekuwa kiungo wa SC Villa Mganda, Kenneth Semakula ili kujiunga nao msimu ujao.

Uongozi wa Simba unaamini kiungo huyo wanaweza kumpata kwa gharama ndogo kwa sababu ni mchezaji ambaye yupo huru sokoni na wanamuona ataleta tija kikosini humo baada ya kutokuwa na matumaini na Msenegali, Babacar Sarr.

Kennedy kutua Coastal Union

WAGOSI wa Kaya, Coastal Union wameanza hesabu za kumnasa beki wa Simba, Kennedy Juma baada ya nyota huyo mkataba wake kumalizika msimu huu.

Hatua ya Coastal inatokana na kuondokewa na beki wa kikosi hicho, Lameck Lawi ambaye tayari msimu ujao atajiunga na Simba baada ya kufikia makubalino baina ya timu hizo na kusainishwa kandarasi ya miaka miwili.

Mkenya aingia rada za Ihefu

KLABU ya Ihefu, inawania saini ya kiungo mshambuliaji wa Gor Mahia, Austin Odhiambo kwa ajili ya kujiunga nayo msimu ujao.

Taarifa zinaeleza nyota wawili wa Kenya, Elvis Rupia na Duke Abuya ndio ambao wanatumika kama chambo cha kumshawishi kiungo huyo japo changamoto kubwa inayoweza kutokea ni kutokana na Gor Mahia kufuzu Ligi ya Mabingwa.


ERICK Johora haendi kokote

UONGOZI wa Mashujaa, umeanza mazungumzo ya kumpa mkataba mpya kipa wa timu hiyo, Erick Johora ili kuendelea naye msimu ujao.

Kipa huyo aliyejiunga na timu hiyo Januari mwaka huu akitokea Geita Gold, mkataba wake wa miezi sita umemalizika na yupo huru.

Awali, kipa huyo wa zamani wa Yanga, alipewa mkataba mpya ingawa aligoma kusaini kwanza.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz